Kila tarehe 6 Januari, Kanisa linasheherekea Siku kuu ya "Toleo la Bwana" inayotambulika kama Epifania. Hii ni Sherehe ambayo
Mfalme Masiha anajitambulisha wazi katika Ulimwengu. Injili ya Mathayo 2:1-2 inazungumzia Mamajuzi waliofuata
mwongozo wa nyota ili wakamwone Masiha na kumsujudia. Ni kwa njia ya nyota, Mamajusi wanaweza kufika
mahali alipokuwa na wakaweza kumsujudia na kumpatia zawadi zao. Kumbe Yesu
Kristo Masiha ni nyota inayaangaza na kuongoza maisha yetu mpaka mwisho wa
nyakati hadi kufika mbinguni. Katika Siku kuu ya Krismasi tarehe 25 Disemba,
Kristo anajitoa katika watu ulimwenguni. Siku kuu ya Toleo la Bwana yaani
"Epifania" Mamajusi wanawakilisha watu wote ulimwenguni wanaojitolea
kwa Bwana kwa kumwabudu, kumwamini na kumsujudia
No comments:
Post a Comment